- Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Africa Mashariki
Tuwezesha kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
- Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Na tulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
- Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa haki na mali
Tuijenge Jumuia bora.